SAFARI YANGU ni riwaya ya Kiswahili inayoyateka na kuyaakisi maisha ya vijana wengi wanaotamani kufanikiwa maishani kwa njia ya mkato. Mwandishi amejaribu kutumia ufundi wa lugha kwa kuimulika jamii yake na kuyaibua mambo yanayowasibu vijana wengi wa sasa. Zaharani anatamani kuishi Ulaya akiamini kuwa huko ndiko kwenye pepo ya dunia. Anajenga mazoea na mgeni wa kizungu (Eliza) aliyekuja kijijini kwao kwa ajili ya utafiti wa mambo ya misitu na vyanzo vya maji. Eliza anaamua kugharamia safari ya Zaharani ili aishi Ulaya. Hali tete inamkabili Zaharani baada ya mchumba wa Eliza kubaini kuwa Eliza...
SAFARI YANGU ni riwaya ya Kiswahili inayoyateka na kuyaakisi maisha ya vijana wengi wanaotamani kufanikiwa maishani kwa njia ya mkato. Mwandishi ameja...