Katika sehemu ya kwanza na ya pili ya kitabu, Chachage anafanya uchambuzi wa kina wa mfumo wa utandawazi na soko huria. Makala yake juu ya zao la tumbaku na korosho yanadhihirisha wazi madhara yaliyowapata wakulima wadogowadogo katika soko huria, kwa maana nyingine, anaelezea juu ya uhuru waliopewa wafanyabiashara wanunuzi wa mazao ya wakulima bila usimamizi wa serikali. Kwa ustadi mkubwa, msomi wetu pia anachambua nafasi na hali ya wachimbaji wadogowadogo na jinsi wawekezaji katika migodi wanavyochuma rasilimali zetu bila kunufaisha nchi wala wazalishaji wadogo. Jambo hilo siyo geni. Hivi...
Katika sehemu ya kwanza na ya pili ya kitabu, Chachage anafanya uchambuzi wa kina wa mfumo wa utandawazi na soko huria. Makala yake juu ya zao la tumb...