Bw. Godwin Chilewa alizaliwa wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro. Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Kichangani iliyopo mjini Kilosa na baadae katika shule ya sekondari Kibasila iliyopo jijini Dar es Salaam. Bw. Godwin amehitimu stashahada ya upelelezi kutoka School of Criminal Investigation (USA), shahada ya uongozi katika chuo kikuu cha Ashworth, shahada ya Saikolojia kutoka University of Houston Downtown, na shahada ya uzamili (MBA) kutoka Devry University Houston, Texas