ISBN-13: 9781499199352 / Swahili / Miękka / 2014 / 68 str.
Mathias E. Mnyampala (1917-1969) is a famous Tanzanian lawyer, writer and poet who wrote in Kiswahili. The unpublished manuscript of his autobiography has been discovered in 2007 in Dodoma (United Republic of Tanzania) by Dr Mathieu Roy by finding the heir of the author. Roy then edited the manuscript for the first time in 2013. It was conserved in Dodoma with other unpublished manuscripts and rare literary archives by Charles M. Mnyampala, the second son of the author who received from his father the mission to conserve and publish these precious documents since 1969. This Kiswahili book is a light edition from the main paper book and contains only Mnyampala's autobiographical text with an introduction by Charles M. Mnyampala. Marehemu Mathias E. Mnyampala (1917-1969) aliandika habari za maisha yake wakati alipokuwa ameshaona kwamba anakomea mwisho wa uhai wake kutokana na kuumwa sana na ndwele miaka 1968-1969. Wakati huo alikuwa ameshakuza sana lugha ya Kiswahili kwa ufasaha wake wa kishairi na mambo mengine mengi pamoja yake vitabu vyake kuhusu historia ya Ugogo, siasa ya Ujamaa, dini na maisha ya wafu maarufu kama Mtemi Mazengo na Sheikh Kaluta Amri Abedi. Kwa sababu kumbe alifanikiwa sana kutoka utoto wake katika machunga ya Ugogo, bila kujua kusoma wala kuandika hadi umri wa kuoa mke na kulipa kodi, mpaka ubingwa wa lugha ya Kiswahili na utungaji wa idadi ya vitabu inayozidi ishirini na tano akiwa anadhaniwa na wataalamu wa ushairi wa Kiswahili na washairi wenzake wenyewe kuwa malenga mmoja mkuu wa Karne iliyopita. Alikuwa mzalendo mkubwa wa Taifa la Tanzania na alijitolea kabisa kueneza lugha yake Kiswahili maisha yake yote. Mchango wake Mathias E. Mnyampala kwa fasihi ya Kiswahili na Taifa lake ni tukufu, kadiri ya kupewa heshima kubwa ya Nishani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Rais Ali Hassan Mwinyi mwaka 1994. Mswada huu ambapo marehemu Mathias E. Mnyampala anatusimulia habari za maisha yake binafsi ulibaki muda mrefu sana uliozidi miaka arobaini bila kupigwa chapa. Uligunduliwa mwaka 2007 mjini Dodoma na Dr Mathieu Roy na kupata kuhaririwa mwaka 2013. Mswada ulikuwa unahifadhiwa kwa makini sana na Charles M. Mnyampala, mtoto wa pili wa Mathias E. Mnyampala, kuanzia kifo cha baba yake mwaka 1969. Kwa mara ya kwanza, toleo hili kutoka shirika la DL2A - Buluu Publishing (Ufaransa) linawapa wasomaji watukufu na wapenzi wa Kiswahili nafasi ya pekee ya kugundua maisha ya mzungupule huyo wa Kiswahili na fasihi yake. Toleo hilo lenye bei nafuu limepunguzwa picha na kurasa kadhaa ukilingana na toleo kuu la kwanza. Mswada wote wa Maisha ni kugharimia ulinukuliwa kwa ukamilifu.